Ujenzi wa daraja la chuma la muda la mto pangani umefikia asilimia 25% kukamilika kwake ili kuanza ujenzi wa daraja la mtopangani ambao utagarimu Zaidi ya bilioni 82 hadi kukamilika kwake.
Akitoa taarifa mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la mto pangani Mkuu wa wilaya ya pangani zainab Abdala kwa mwenyekiti wa Chaman cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajab Abdulhaman Abdala amesema kuwa mradi huo hadi kukamilika utachukua miezi 36 na utagharimu kiasi Zaidi ya bilioni themanini na mbili hadi kukamilika kwake ,ambapo utasaidia wananchi wengi kuondokana na changamoto kivyuko pindi kinapo harika nahivyo kuwakwamisha katika shuhuli zao za kila siku za kujipatia kipato.
Aidha kwaupande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Tanga MNEC Ustadh Rajab Abdulhaman Abdalah, amesema anashangazwa na wanaochukia sifa zinazotolewa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani ni muhimu wafike katika miradi inayotekelezwa na serikali wapate cha kusema nasio kubedha.
“Mara zote tunapompongeza na kumsifu mheshimiwa Rais wetu wengine huwa hawatuelewi na ili waelewe wafike site (eneo la mradi) waone anachokifanya kutekeleza ilani ya chama chetu,” alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema Chama cha Mapinduzi wakati ule kikinadi ilani yake na kuanisha miradi mbalimbali wapinga Maendeleo ambao ni wapinzani walisema hayatawezekana jambo ambalo lilikuwa si kweli.
Awali akisoma utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo mradi unaotekelezwa na kampuni ya Ms Shandong Luqiua Group ya Kichina, Mhandisi wa Tanroad Mhandisi Safia Maliki Alisema serikali itaigharamia mradi huo kwa asilimia 11.16 na benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa fedha kwa asilimia 88.84.
Alisema mradi huo ulioanza Desemba mwaka jana na hadi kufikia mwezi huu utekelezaji wake umefikia asilimia 5 kwa kazi mbalimbali zimefanyika ikiwemo ujenzi wa daraja la muda katika daraja hilo.