Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham amewataka vijana waendesha bodaboda wilayani humo kuunda vikundi kwaajili ya kuchangamkia fursa mbalimbali za kimaendeleo zilizopo ili waweze kukuza uchumi wao.
Mbunge Salim ameyasema hayo wakati wa kukabidhi reflector kwa bodaboda hao ili kuwafanya watambulike rasmi na kuepusha Vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na watu wanaojifanya ni bodaboda katika wilaya hiyo.
Aidha mbunge amewaahidi madereva hao wa bodaboda kuwaandalia mafunzo maalum ya udereva ili wapatiwe vyeti vitakavyowasaidia kupata leseni kutokana na Changamoto ya sasa ya madereva wengi kutokuwa na leseni.
Kamanda wa jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani wilaya ya Ulanga JOSEPH ISAGALA amemshukuru Mbunge Salim Alaudin Hasham kwa kuwapatia bodaboda reflector hizo na amewataka bodaboda hao kufuata sheria za usalama Barabarani na wajitokeze kwa wingi kipindi ambacho mafunzo maalum ya sheria hizo yatakuwa yanatolewa.
Elia Tirani na Clement liyengejele ni viongozi wa bodaboda wilaya ya Ulanga wamemshukuru Mbunge kwa kuwapatia reflector hizo na wamemuahidi kuwahamasisha vijana kushiriki kwa wingi mafunzo ya sheria za Barabarani ili wapate leseni ambazo zitawaepusha kukamatwa mara kwa mara na askari wa usalama Barabarani.
Aidha viongozi hao wa bodaboda wamemuomba Mbunge kuwawezesha mikopo ya pikipiki ili wawezekujikwamua wao wenyewe kwani pikipiki walizonazo kwasasa si zao hivyo zinawafanya wanashindwa kujiinua kiuchumi badala yake wanatafuta fedha ya boss pekee.
Mbunge Salim amewasisitiza kutengeneza vikundi imara ili pindi atakapotaka kufanya jambo lolote kwaajili ya bodaboda iwe rahisi kutekelezeka kwani watakuwa imara na wenye uhitaji wa kweli.
Jumla ya bodaboda 324 wamepatiwa reflector hizo katika mno wa mahenge na zoezi hilo litaendelea kwa jimbo zima la Ulanga ili kuendana sambamba na sera za usalama Barabarani.