Ni June 19, 2023 ambapo kumefanyika mjadala wa kitaifa ambapo ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Ubunge Prof Kitila Mkumbo, Mfanyabiashara Rostam Aziz, Jenerali Ulimwengu pamoja na wadau mbalimbali.
Mjadala huo uliowakutanisha watu wao katika ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam, Mada kuu ni kulinda kuendeleza Umoja wa kitaifa wakati wa Mageuzi ya kisiasa na Kiuchumi.
Hapa nimekusogezea nukuu ufahamu kile alichozungumza Mbunge Jimbo la Ubungo, Prof Kitila Mkumbo.
“Bunge lilipitisha nini pale Bungeni Dodoma? Watani zetu kwa maana ya wapinzani wanajenga hoja kuwa CCM inauza Bandari. Hilo suala kwa sasa linaanza kueleweka kuwa hakuna suala la mauzo sio tu Bandari bali sehemu yoyote ndani ya nchi haiwezi kuuzwa,”- Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo.
“Makubaliano yalihusu uendelezaji na uboreshaji na sio uuzwaji wa bandari. Kwa sasa kinachozungumziwa ni uboreshwaji wamagati saba kama gati la magari, gati la mizigo mchanganyiko, gati la makontena, gati la majahazi na abiria, n.k.”- Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo.
“Kampuni ya DP World ikija lazima isajiliwe Tanzania kwa kufuata Sheria zote za Tanzania. Hata bila mkataba, endapo kutatokea tatizo basi Sheria za Tanzania zitachukua hatua- Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo.
“Hoja za majadiliano ya mkataba wa bandari zimejadiliwa kwa kina na watu wenye uzoefu mkubwa, hivyo kamwe Wabunge wasingeingia mkenge kwa kupitisha kitu kisichokuwa na tija kwa Taifa. Watanzania wana hofu na mali zao, ni jambo jema kwao. Tanzania ipo sheria kuwa mikataba ikisainiwa inaweza kuletwa ili kuipitia kwa kina kwa manufaa ya Taifa,”- Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo.
“Nchi yetu ina dini na makabila lakini hayo tulikubaliana kuyaepuka kwa manufaa ya nchi yetu. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pande mbili ambazo ni kitu kimoja. Viongozi wasihukumiwe kwa sababu ya tofauti zao za dini, ukabila, ukanda na rangi. Kwenye uwekezaji kuna mbinu mbili ambazo ni uzalendo wa kiuchumi na uchumi wa kizalendo,” – Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo.
“Kwenye mambo ya mikataba ya uwekezaji kuna mambo matatu muhimu ambayo wabunge tuliyaangalia na sio hili la mauziano kama inavyosemwa mtaani ila uendelezaji na uboreshaji ambao kwetu ndio kitu muhimu tulichoangalia. Hivyo niseme hapa kuwa yaliyojadiliwa bungeni ni makubaliano sio mauziano,” Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo.
“Kitendea kazi cha mbunge ni hisia na maoni ya Watanzania ili kuangalia tija kwa nchi yetu. Maeneo ambayo yamejadiliwa na Watanzania nje ya Bunge, kabla ya mkataba kupitishwa, yataangaliwa kwa kina. Watanzania na wote wanaofanya kazi bandarini wataangaliwa kwa kina juu ya ajira zao. Kama viongozi tuna dhamana ya kitaifa ya kulinda, amani, umoja na mshikamano kama nchi,” Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo.