Ni June 19 ,2023 ambapo Mkurugenzi mpya wa jiji la Dodoma, John Kayombo amekabidhiwa ofisi pamoja na nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Joseph Mafuru.
Kabla ya uteuzi huo Kayombo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa miaka miwili, pia alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Kayombo pia alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa miaka mitatu.