Msimu mpya uzalishaji Kilombero kuzalisha zaidi Tani laki moja
Share
2 Min Read
SHARE
Kampuni ya Sukari Kilombero ilizindua msimu wa uzalishaji kwa mwaka 2023/24 katika moja ya viwanda vyake (K1) kwenye hafla iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe Dunstan Kyobya.
Hafla hiyo fupi, imefuata baada ya ufunguzi wa msimu wa kiwanda cha K2 uliofanyika tarehe 14 Juni 2023 ukiashiria kuanza kwa kipindi muhimu cha uzalishaji wa sukari, ambapo kampuni inatarajia kuzalisha tani 129,080 za sukari kwa msimu.
Kufuatia uzinduzi wa msimu wa uzalishaji, kampuni pia itachangia katika kuzalisha fursa za ajira za msimu, kwa kuajiri wafanyakazi wa ziada kutokana na ongezeko la kazi katika msimu wa uzalishaji.