Shilole kasimulia alivyowahi kuweka hati Ya Nyumba rehani ili apate hela ya kulipia watoto wake Ada ya shule kwani iliwahi kufika mahali alikuwa anapambana na bado anajikuta anakosa Hela ya Ada mpaka kutumia njia nyingine za kiupambanaji.
Shishi amezungumza hayo kwenye mahojiano na AyoTVENT leo hii katika ofisi zake za Shishi Food ikiwa ni masaa machache baada ya kutangaza furaha aliyonayo baada ya mtoto wake Joyce kufaulu Devision 1 ya 7 kupitia matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo.
Katika hatua nyingine shilole ametangaza ujio wa Festival yake ya vyakula vya asili itakayokuja hivi karibuni baada Ya kuanzisha Mtindo wa kupika vyakula vya kiasili vya kila makabila Kwa kila siku ya Alhamis na alianza na Wachaga huku week hii akipika vya Wahaya.