Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao Julai 12, 2023 amepokea Wananchi kutoka CUF 10, UDP 1 Jumla 11 katika kata ya Mahege Wilaya ya Kibiti katika Mkoa wa Pwani, Tanzania.
Aidha Pia ameshiriki katika Uchaguzi mdogo Kata ya Mahege ambapo Matokeo yakatangazwa Julai 13, 2023 yafuatayo.
Kura Zilizopigwa: 1118
Kura Zilizoharibika: 30
Kura Halali: 1088
1. CCM : 928
2. CUF. : 133
3. UMD : 06
4. UDP. : 06
5. UPDP : 06
6. NRA : 03
Ndipo Bw Hamada. J. Hingi atangazwa kuwa mshindi wa Udiwani kata ya Mahege kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Baada ya Chaguzi hizo kufanyika Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao alizungumza haya mbele ya Wananchi wa kata hiyo ya Mahege akimuagiza Diwani kuyatekeleza yale yanayohitaji kwa Jamii.
‘Wananchi hawa watakwenda kuamini Chama cha Mapinduzi kwa kukuchagua wewe, sisi tumekuja hapa kuweka maagano baina yetu na Wananchi wa kijiji hiki, wamekuchagua wewe na watakuwa wameichagua CCM hilo Wananchi hawa watapata maendeleo kupitia CCM kutoka kwako wewe’ – Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao
‘Yapo mambo yaliyofanywa na Diwani aliyepita kwahiyo wewe utaenda kuendeleza yale yaliyoachwa, usiende kutuangusha nenda katekeleza yale yaliyo bora yale Wananchi wanayohitaji, naamini mpaka 2025 hakutakuwa na Changamoto yoyote kazi yako kuhakikisha majukumu yote unayatimiza’- Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao
‘Lakini inadaiwa katika Kijiji hiki kuna kitongoji hakina Umeme kwahiyo hayo ni sehemu ya Majukumu yako wewe kuhakikisha mpaka kufika Mwaka 2025 Umeme kwao uwe umewaka na Mheshimiwa Mbunge ananisikia hapa, wewe ndio Diwani Mkuu ambae utahusika nae kwenda kutatua matatizo ya Wananchi ‘- Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao
Lakini pia Mwenyekiti wa Chama wa Kata amenieleza kwamba hapa yapo Majengo matatu hayajakamilika na yamejengwa kwa nguvu ya Wananchi yanahitaji kukamilika hivyo nenda kasimamia na ukahakikishe yanakamilika, CCM ni chama ambacho kikiahidi kinatekeleza hivyo kasimamie misingi imara ya Chama’- Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao
Aidha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao katoa Katoa Tsh 1,000,000/- kusaidia Kampeni za CCM kata ya mahege na pia kahimiza Wananchi kutunza miradi iliyopo ili isaidie kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu.