Waimbaji Mastaa Alikiba autambulisha wimbo Wake wa Sumu aliomshirikisha msanii Marioo Kwa style Ya kitofauti kwa kualika baadhi ya wadau na watu maarufu waliopo Kwenye muziki wa Bongofleva kusikiliza wimbo huo maeneo Ya Mbezi beach Daresalaam
Alikiba na Marioo wamealika wakali wa ticktock, wasanii, Dancer na waandishi wa Habari ambao wote walifika Kwa lengo la kusikiliza wimbo huo wenye mahadhi Ya kiamapiano
Baada Ya utambulisho wamefunguka Kwa Pamoja na Alikiba amesema “Ni chemistry iliyonyooka, kila kitu kinawakati Wake na marioo ni mdogo wangu, alikuja Nyumbani alitamani tufanye wimbo na hatimaye Ndio huu, Sio kwamba si support muziki wa amapiano, muziki ni muziki, sijachukia amapiano nilijiwekea tu, niliweza kufanya amapiano lakini nilimpa Abdukiba autumie ‘Hainogi’ ule wimbo ulitakiwa kuwa Kwenye Album yangu lakini nilimpa Abdukiba akaufanya, amapiano Ni muziki rahisi sana kufanya”
Marioo yeye amesema “Alikiba anapenda muziki mzuri, kazaliwa anafanya muziki mzuri, nilimuuliza kuwa nasikia amapiano haufanyi akasema mimi Sound yoyote nafanya ilimradi muziki mzuri”
Full Interview iko YouTube Ya #millardayo