Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu Jijini Dar es salaam leo July 26,2023 ambapo amewasihi Viongozi wenzake kuwekeza kwenye kuinua maisha bora ya Watu ili Vijana wapate maisha bora hapahapa Afrika na wasilazimike kwenda Ulaya kutafuta maisha bora.
“Lazima tujidhatiti kutumia rasilimali Watu tuliyonayo kwa manufaa yetu, idadi kubwa ya Vijana Afrika ni fursa pekee ya mageuzi ya kiuchumi, badala ya kuwaacha Vijana hawa wavuke Bahari, wapigwe njiani wazamishwe kwamba wanakwenda Ulaya kutafuta maisha bora, maisha bora watayapata Afrika tukiwaendeleza”
“Lazima tuwafundishe Watoto wetu pia kuhusu uzazi wa mpangilio, kama nilivyosema Afrika population yetu ni kubwa na inaweza kutupa tija au inaweza kutuletea mambo yasiyofaa kama hatukuitumia vizuri”
“Tuhakikishe pia elimu tunayotoa inawapa uwezo Vijana wetu kuongeza tija na kujenga uchumia, pia tuongeze uwekezaji kwenye sekta nyingine zinazoleta ufanisi katika huduma za elimu na afya, tuwekeze kwenye njia za usafiri na usafirishaji, maji, umeme, usafi wa mazingira n.k”