Kampuni ya kimataifa ya Future Face kwa kushirikiana na Mwanamitindo Mtanzania Millen Magese imetangaza kufanya usahili wake kwa mara ya kwanza Nchini Tanzania kumsaka Mwanamitindo mmoja wa Kitanzania mwenye umri kati ya miaka 16 hadi 25 atakayeiwakilisha Nchi kwenye shindano kubwa la Afrika litalosaka Wanamitindo wa kwenda kufanya kazi hiyo katika Nchi mbalimbali zikiwemo za Ulaya.
Taarifa iliyotolewa na @LadivaMillen ambaye ndiye Msimamizi Mkuu kwa upande wa Tanzania imesema mwaka huu Tanzania imepata nafasi hiyo ya usahili kwa mara ya kwanza ambapo Wanamitindo watashindania kupata mkataba wa miaka miwili ya uwanamitindo kimataifa kwenye miji kama New York, London na Milan.
Usahili wa Tanzania utafanyika Jumapili ya August 6 Warehouse, Masaki Jijini Dar es salaam kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na moja jioni ambapo yeyote mwenye kutaka kushiriki anaweza kujisajili kuanza sasa kupitia www.futurefaceglobal.com
Millen amesema baadhi ya Models waliopitia mikononi mwa FUTURE FACE wamefanya kazi na Brands bora kama vile Victoria’s Secret, Tom Ford, Chanel, Fenty, Fendi, Burberry, Dolce na Gabbana, Calvin Klein, Ralph Lauren, Moschino, GQ Magazine, Alexander McQueen, Vogue, Dior, Gucci, Balmain, Gucci, Prada, YSL, Rick Owens, Hermes na wengine wengi. #MillardAyoUPDATES