Katika kuadhimisha miaka 56 ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Bara la Asia (Asean), Balozi wa Indonesia Tri Yogo Jatmiko amesema watahakikisha wanaongeza ushirikiano baina ya Afrika Mashariki na jumuiya hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho hayo, Balozi Yogo amesema..”Hii ni mara ya pili kufanyika kwa jambo hili hapa Dar es Salaam ikiwa ni Wanafamilia wa Asean ambapo tupo wawakilishi wawili sisi Ubalozi wa Indonesia na Vietnam lakini wapo wengine wengi”
“Haya maadhimisho ni muhimu kwetu hasa kwa Wanajumuiya kukutana ambapo jukwaa hili litasaidia kutatua changamoto ba kuongeza ushirikiano kati yetu,
“Tunafanya haya kwa ajili ya kuitangaza jumuiya yetu Dar es Salaam na Afrika kwa sababu moja kati ya changamoto tunayokutana nayo watu wengi wa Afrika Mashariki hawaijui historia zaidi ya Aesian na Aesia hawaijui ya Afrika Mashariki hivyo hii itasaidia kutangaza na kuongeza ushirikiano,” Amesema Balozi Yogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza amesema
“Hii shughuli ya michezo kwa Wanafamilia wa Indonesia na balozi nyingine za Asean ambao ni umoja wa nchi za Kusini mwa Bara la Asia zipo nchi 11,”.
“Leo ni siku ya maadhimisho tangu ianzishwe hii jumuiya wametimiza miaka 56 ambapo katika kuadhimisha tangu kuanzishwa kwake wameona wafanye shughuli ya michezo kama hii na sisi tunatarajia kuzidisha ushirikiano zaidi katika sekta mbalimbali ikiwemo kiuchumi,”.