Sasa ukiacha na mafanikio yao hauwezi kuacha kumtaja muwekezaji namba moja GSM yaani mdhamini Mkuu na kupitia documentary yao wamempa nyota tano mabegani ikiwa kama ishara ya kumpa pongezi kwa kuendelea kuwa mdhamini mkuu katika klabu hiyo.
Aidha Ghalib Said Mohamed aliweza kuzungumza machache na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa documentary hiyo na kusema…’Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza Young Africans kwa mafanikio Mwaka 2022/23 kwa kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii, Ubingwa wa Ligi Kuu, Ubingwa Azam Sports Federation CUP na kufika fainali ya CAF hakika haya ni mafanikio makubwa ya Club yetu’
‘Sasa hivi wanaelekea kuanzia msimu 2023/24 naamini Yanga Bingwa tena rekodi inaenda kuandika kama mlivyoshuhudia kile kilichopo kwenye Documentary ili vizazi na vizazi waje kujua mengi kuhusu Young Africans basi hivyo hivyo tunaenda kuiandika rekodi nyingine katika msimu huu mpya na inshallah Mwenyezi Mungu atupe umri na Afya tele tukutane hapa hapa kushuhudia Documentary ya msimu wa 2023/24 Yanga Bingwa’- Mkurugenzi na Rais wa GSM, Ghalib Said Mohamed