Leo imesambaa picha mchezaji wa Yanga Djuma Shaban Raia wa Congo DR akiwa na jezi za mazoezi za Azam katika uwanja wa Azam Complex Chamazi akifanya mazoezi.
Picha hiyo imekuwa gumzo na kuhoji kunani, Yanga bado hawajatangaza kumuacha au kumuuza lakini Azam FC pia hawajasema kama wamemsajili au la, Mkuu wa idara ya habari ya Azam FC Thabeet Zacharia (Zakazakazi) ameweeleza ukweli wa picha hiyo.
“Djuma Shaban yupo na Azam FC kwa muda mrefu tu sasa akifanya mazoezi kwa ajili ya kulinda kipaji chake, alikuja akaomba na akakubaliwa akawa anafanya mazoezi na sisi alisema hana timu kwa sasa ameshaachana na Yanga kwa ajili ya kulinda kipaji chake inabidi apate sehemu ili akipata timu asiwe na shida sana”>>> Thabeet Zacharia Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Azam FC