Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa amesema kuwa kwa kasi ya maendeleo inayofanywa na Mhe. Dr. Hussen Ali Mwinyi na Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassani CCM lazima ishinde kwa kishido katika uchaguzi ujao katika visiwa vya Pemba na Zanzibar kwa ujumla.
“kuna watu wamezoea na ndivyo wanasema eti CCM haikubaliki Pemba laasha kwa speed ya maendeleo inayoletwa na Dr. Mwinyi na Dr. Samia, kwa lazima ushindi utakuwa wa CCM.” Rehema Sombi
Aidha amesema kuwa Kabla ya Mapinduzi ya januari 1964, wananchi walikua hawashirikishwi katika katika maamuzi kuhusu ustawi wa maendeleo yao. Mtiririko wa ngazi za utawala ulikua ni wa kupokea amri na kusimamia utelezaji wa amri hizo ambazo huanzia ngazi ya juu ya utawala na kuteremshwa hadi ngazi ya chini kwa wananchi na jamii kwa ujumla. Maamuzi ambayo hayapigwi wala kujadiliwa na wananchi wa kawaida ila ni utekelezaji tu.
Lakini Leo hii wananchi wanashirikishwa kwenye maamuzi ya nchi yao, wanashirikishwa katika maendeleo ya nchi yao.
Pamoja na hayo ameleza kuwa Serikali imeenda mbali zaidi mpaka kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa jambo ambalo lisingewezeka na kabla ya mapinduzi.
Ameongezea kuwa kwa uungwana wa Serikali za CCM ilikubaliana kuwepo serikali ya umoja wakitaifa, pamoja na CCM kuongoza wingi wa viongozi katika vyombo vya maamuzi lakini kwakuwa lengo ni kujenga nchi moja CCM ilikubaliana na hili na limeleta manufa zaidi ya kujenga nchi kuleta maendeleo kwa utulivu mkubwa.
“Tunaijenga nchi yetu kwa pamoja, tunakosoana tunarekebisha na mwisho wa siku tukubaliana kwenye ujenzi wa nchi yetu.” Amesema Rehema Sombi
Hata hivyo ameongezea kwa kusema kuwa wPamoja na maendeleo makubwa yanayoletwa hapa Zanzibar ususani Pemba Wako watu wa Chache hapa wanachokonoachokonoa hawataki maendeleo makubwa yanayofanywa na wameenda mbali wanataka kuvuruga muungano wetu lakini kwa uimra wa Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan na Mhe. Dr. Hussein Mwinyi jambo hilo alakuvunjika kwa muungano alitakaa litoke.
“Nataka niwambie msikie na muwafikishie hao wache kuwa Chama Chetu kitadumu, moja wetu utadumu na muungano wetu utadumu na Afrika itaendelea kuwa huru na itadumu” Rehema Sombi
Makamu Mwenyeki wa UVCCM ameyasema hayo Leo tarehe 9 septemba, 2023 katika mkutano wa adhara visiwani Pemba katika kuitimisha ziara ya Kamati ya utekelezaji ya UVCCM inayoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Mohammed Kawaida.