Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wahandisi utakaohusisha mambo mbalimbali pamoja nakuwasajiri wahandisi 45.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es laammsajili wa bodi ya usajili wa wahandisi Mhandisi Bernard Kavishe amesema kukutana huko ni maalum kwa ajili ya kupokea maelekezo ya serikali.
Amesema shughuli za kijamii zitakuwepo ikiwemo kuchangia damu salama.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mhandisi Benedict Mukama akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutakuwepo na wageni wa ndani na nje ya nchi.