Licha ya Serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini, Bado kumetajwa uwepo wa changamoto ya baadhi ya sheria kukinzana kati ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na taasisi za udhibiti zinazojishughulisha na usajili wa biashara na leseni za taasisi na kampuni mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Taasisi za Udhibiti, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema kuwa changamoto hizo zinaathiri mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Wananchi.
Amesema bado wananchi wanahitaji elimu juu ya usajili wa majina ya kampuni na. Umuhimu wake ili iwe rahisi katika kuthibiti muingiliano wa umiliki halali wa majina .
Chanzo cha changamoto hizo imeeelezwa kuwa ni uwepo wa taasisi zaidi ya moja zinazojihusisha na usajili wa taasisi na kampuni mbalimbali nchini bila uwepo wa muongozo maalumu wa sehemu ya kuanzia.