Naibu Waziri wa Uchukuzi David Mwakiposa Kihenzile amesema Shirika la Reli Tanzania (TRC) linatakiwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo ili kuongeza pato la Taifa, pia Shirika linatakiwa lihakikishe kuwa miundombinu na vifaa vya uendeshaji vinavyonunuliwa vinaendana na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali na muda wa mikataba ya miradi mbalimbali uzingatiwe ili uendeshaji uanze kwa wakati.
Kihenzile amesema hayo alipotembelea Makao Makuu ya TRC na kufanya kikao kifupi na Menejimenti ya TRC kwa lengo la kujitambulisha na kujionea kazi zinazofanywa na TRC ili kupata uelewa utakaomsaidia katika kutekeleza majukumu yake ndani ya Wizara.
Kihenzile amesem muda wa mikataba ya miradi mbalimbali unapaswaa pia uzingatiwe ili uendeshaji uanze kwa wakati, Mwenyezimungu ametujaalia nchi ambayo ina jografia nzuri, tuna bandari inayotegemewa na nchi nyingi zinazotuzunguka, suluhisho la kuwafikishia mizigo yao kwa haraka ni SGR”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Amina Lumuli amesema Wakandarasi wanaendelea na kazi kwenye vipande vyote vitano ya ujenzi wa SGR awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam hadi Mwanza na vilevile ujenzi huo wa SGR kwa awamu ya pili una vipande vinne, kipande cha kwanza kutoka Tabora – Kigoma chenye urefu wa kilometa 506 mkandarasi ameshaanza atua za awali za ujenzi, na vipande vilivyobaki tayari umeshafanyika usanifu wa awali na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuanza ujenzi.
“Mradi wa SGR umetoa ajira zaidi ya laki moja za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Watanzania na kuwa chachu ya uchumi kwa Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”