Kufuatia uhaba wa maji katika Mji Mkuu wa Africa Kusini Johannesburg, Wasambazaji wa maji wamewataka wakazi wa Jiji hilo na Vitongoji vyake kutumia maji kwa kiasi kwa kutumia dakika mbili kuoga na kuosha magari yao kwenye siku za wikendi pekee tena kwa kutumia ndoo huku wakiwasihi Watu kuepuka kumwagilia bustani na nyasi kwa maji safi.
Kampuni ya Rand Water na Johannesburg Water ambazo zinasambaza maji zimesema matumizi makubwa ya maji kwa Wakazi wa Jiji hilo yanatatiza mfumo mzima na kusababisha maji kuzidi kupungua kwenye hifadhi yake hivyo zimewataka Watu kuokoa maji kwa kutoa pia taarifa kuhusu uvujaji wa maji.
Johannesburg kwa sasa inapitia changamato ya uhaba wa maji inayotokea kila mwaka ambayo mara nyingi hutokea wakati wa kiangazi cha Afrika Kusini kati ya September na mwezi March, katika Wiki za hivi karibuni, baadhi ya Wakazi wa Jiii hilo na Taasisi kama vile Hospitali zimekosa maji na kusababisha Wananchi kupaza sauti wakieleza kutoridhika na hali hiyo.