Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Nachingwea – Ruangwa – Nanganga, sehemu ya Ruangwa – Nanganga (KM 53.2) inayojengwa kwa kiwango cha lami, leo September 18, 2023.
Rais amesema Serikali ya awamu ya sita imejipanga kujenga miundombinu ya Mikoa ya Kusini ili kurahisisha usafirshaji wa mazao na kukuza uchumi wa Mikoa hiyo na kuwataka Wakandarasi wakamilishe ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati.
“Niwaombe Wakandarasi na Wasimamizi waende kwa kasi sana lakini nipongeze TANROADS Mkandarasi na wengine kwa hatua ambayo imeshafikia na kwetu sisi Serikali mafedha yapo tunasubiri certificate ziletwe tulipe kazi ziendelee”
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta, amesema Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ni China 15th Group kwa thamani ya Tsh. bilioni 50.3 na jumla ya Tsh. bilioni 1.1 ikiwa ni sehemu ya ongezeko la thamani na kutumika kulipa fidia ya mali na ardhi kwa Watu walioathirika na ujenzi kwa mujibu wa Sheria “Ujenzi mpaka sasa tumefikia 71% na mapaka sasa tumeshalipa jumla ya shilingi Bilioni 20.7 na zilizobaki tunaendelea kulipa kwa utaratibu uliowekwa”