Ni Afisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe ambapo leo Septemba 18, 2023 amekutana na vyombo vya habari kuelezea namna walivyojipanga kuelekea mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Namungo Jumatano 20/9/2023.
“Tunashukuru Mungu kwa kurejea salama Tanzania na leo Wachezaji watarudi kambini kuanza maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo, Jumatano ya tarehe 20.09.2023”- Ali Kamwe
“Nahodha wetu Bakari Mwamnyeto ambaye hakuwa nasi kwenye mchezo wa Kimataifa kule Kigali, Rwanda. Leo atarejea mazoezini na wenzake tayari kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo, hautakuwa mchezo mwepesi, kwasababu Namungo ni moja ya timu ngumu kwenye Ligi yetu lakini tuna timu imara na walimu bora”- Ali Kamwe
Mchezo wetu na Namungo utachezwa Jumatano saa 1:00 Usiku, Uwanja wa Azam Complex na Viingilio ni kama vifuatavyo:
Mzunguko – 5,000
VIP B – 10,000
VIP A – 20,000
Na tiketi tayari zishaanza kuuzwa.
“Uongozi wa Young Africans umeutengeneza mchezo wetu dhidi ya Namungo kuwa ni mchezo wa kuwapa maua yao Wananchi wote waliyosafiri kwenda Kigali, Rwanda Dakika ya 12 ya mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya Namungo FC, tutasimama kwa Dakika 1 kuwashukuru Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu yetu waliosafiri kwenda Kigali, Rwanda na kutengeneza historia hii kubwa ya kuwa na Mashabiki wengi kwenye mchezo wa Ugenini”– Ali Kamwe
“Na Viongozi wetu wamewaandalia Surprise kubwa Mashabiki wetu dakika hiyo ya 12 ya mchezo wetu dhidi ya Namungo na hii siyo ya kukosa”