Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (FDA) ilitoa orodha ya bidhaa zilizopigwa marufuku ikiwa ni pamoja na zaidi ya aina 130 za mafuta ya mwili, sabuni na krimu ambazo zina viambato vilivyopigwa marufuku.
Orodha hiyo inajumuisha bidhaa za vipodozi ambazo zina kemikali za kung’arisha ngozi.
Mamlaka hiyo imetangaza kuwa uagizaji na usambazaji wa bidhaa zilizotajwa hautaruhusiwa, lakini pia bidhaa yoyote ya vipodozi ambayo haijatajwa kwenye orodha lakini ina viambato vya kung’arisha ngozi vilivyopigwa marufuku au ina viwango vya juu kuliko vinavyovumilika pia inapigwa marufuku kwenye soko la Rwanda.
Nchini Rwanda kampeni dhidi ya uuzaji na utumiaji wa vipodozi vya aina hiyo imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi, lakini uagizaji na uuzaji wa bidhaa hizo unaendelea kuwepo licha ya kuwa ni kinyume cha sheria.