Mwanamume wa Australia alijaribu kushtaki hospitali ya Melbourne akidai kuwa ‘aliporuhusiwa’ na hata ‘kutiwa moyo’ kuhudhuria sehemu ya tukio la oparesheni ya kujifungua ya mke wake, ambalo limemsababishia kuanza kwa ugonjwa wa akili.
Mnamo Januari 2018, mke wa Anil Koppula alijifungua mtoto mwenye afya njema kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Royal Women huko Melbourne,aliruhusiwa katika chumba cha upasuaji wakati wa utaratibu huo, na alipoona viungo vya mke wake na damu inadaiwa kumesababisha mwanzo wa ugonjwa wa akili.
Sasa, miaka kadhaa baadaye, anajaribu kushtaki hospitali hiyo kwa $ 1 bilioni zaidi ya tsh billion 2 za Kitanzania kwa uharibifu wa kisaikolojia juu yake .
Koppula, ambaye alijiwakilisha wakati wa taratibu za kisheria, alidai kuwa hospitali hiyo ilikiuka wajibu wake wa kumhudumia, na kuongeza kuwa ugonjwa huo wa kisaikolojia ulisababisha kuvunjika kwa ndoa yake.