Mashambulizi dhidi ya kambi mbili za kijeshi kaskazini mwa Mali yanayodaiwa na makundi ya waasi waliojihami yaliwaua wanajeshi watano, huku wengine 11 hawajulikani walipo, jeshi lilisema Jumatatu jioni.
Jeshi lilisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba pia limepoteza ndege wakati wa mapigano katika mji wa Lere, katika eneo la Timbuktu kaskazini mwa Mali.
Takriban washambuliaji 30 “walijitenga” katika shambulio hilo la Jumapili, ambalo jeshi lilisema lilitekelezwa na “magaidi”.
Shirika la Coordination of Azawad Movements (CMA), muungano wa makundi yenye silaha yanayotawaliwa na Watuaregs ambao walichukua silaha mwaka 2012 wakitaka kujitawala au uhuru, walidai kuhusika na shambulio hilo siku ya Jumapili.
Pia ilisema kuwa imechukua udhibiti wa kambi mbili za kijeshi huko Lere na kuidungua ndege ya jeshi.
Lilikuwa ni shambulio la hivi punde dhidi ya vituo vya jeshi kaskazini mwa Mali, ambalo katika wiki za hivi karibuni limeshuhudia kufufuka kwa shughuli za makundi yenye silaha na wanaotaka kujitenga. Mapema mwezi huu, CAM iliteka kambi ya kijeshi huko Bourem, iliyoko kati ya miji ya kale ya Gao na Timbuktu.
TAZAMA PIA ..