Mtanzania Novatus Dismas Miroshi leo amecheza game yake ya kwanza ya UEFA Champions League katika maisha yake akiichezea Shakhtar Donetsk ya Ukraine dhidi ya FC Porto ya Ureno.
Novatus katika mchezo huo alicheza kwa dakika zote 90 licha ya kupoteza kwa kufungwa 3-1, hivyo Novatus sasa anakuwa mchezaji wa tatu katika historia ya Tanzania kuwahi kucheza michuano ya UEFA Champions.
Watanzania wengine waliowahi kucheza michuano hii ni Mbwana Samatta akiwa kama Mtanzania wa pili na Kassim Manara ndio alikuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza michuano hii.