Manchester City wamechagua kutokata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyopokea Rodri wakati wa ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Nottingham Forest Jumamosi.
Hii inamaanisha kuwa kiungo huyo wa kati wa Uhispania atakosa michezo mitatu ijayo ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Rodri alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kuinua mikono yake kwenye koo la Morgan Gibbs White.
Uamuzi wa mwamuzi ulithibitishwa na VAR.
Man City wangeweza kukata rufaa dhidi ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika jaribio la kupunguza adhabu ya Rodri kutocheza mechi tatu.
Lakini gazeti la Daily Mail linaripoti kuwa wameamua kutofanya hivyo, ikimaanisha kwamba atakosa michezo mitatu ijayo.
Mchezo wa kwanza wa kupigwa marufuku kwa Rodri utakuwa wa Kombe la Carabao raundi ya tatu dhidi ya Newcastle Jumatano usiku. Pia atakosa mechi za Ligi ya Premia dhidi ya Wolves huko Molineux Jumamosi kabla na Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates.