Habari ya Asubuhi na karibu kwenye matangazo yetu mubashara hii leo….
Wakala wa Osimhen ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mabingwa hao wa Italia kutokana na chapisho la mtandao wa kijamii la kumkejeli Mnigeria huyo kwa kukosa penalti.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali na talkSPORT, Chelsea wanavutiwa na Osimhen na wanaweza kutumia maneno hayo ya kibaguzi na mzozo huo kuongeza nia yao ya kumpata.
Meneja Mauricio Pochettino ameweka wazi kuwa anataka mshambuliaji mpya mwezi Januari na The Blues pia ni miongoni mwa klabu zinazoonyesha nia ya kumtaka Ivan Toney.
Brentford ingehitaji kima cha chini cha pauni milioni 60 kwa Toney, pia katika orodha ya wachezaji wanaolengwa na Arsenal, lakini hii inatarajiwa kupanda hadi karibu pauni milioni 80 ikiwa timu nyingi zitakuwa kwenye meza.