Balozi wa Ufaransa nchini Niger alisafirishwa nje ya nchi mapema Jumatano asubuhi, vyanzo viwili vya usalama vilisema, karibu mwezi mmoja baada ya serikali ya kijeshi kuamuru afukuzwe.
Utawala wa kijeshi ambao ulichukua mamlaka katika mapinduzi ya Julai ulimwamuru balozi wa Ufaransa Sylvain Itte kuondoka nchini ndani ya masaa 48 mwishoni mwa Agosti kujibu kile walichokiita vitendo vya Ufaransa “kinyume na masilahi ya Niger”.
Lakini amri hiyo hapo awali ilipuuzwa na Ufaransa, ambayo imekataa kuwatambua viongozi wa mapinduzi, na kusababisha maandamano ya kila siku mbele ya ubalozi wa Ufaransa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema mwezi huu kwamba Itte na wafanyakazi wake walikuwa wakishikiliwa mateka katika ubalozi huo.