Mkuu wa wilaya ya korogwe Mh.Jokate Mwegelo amewataka watendaji pamoja na kamati za miradi ya ujenzi kwenye kata na vijiji kufata miongozi ya ujenzi iliyo tolewa na serikali nasio kutumia mawazo yao binafsi kujenga miradi hiyo.
“Rai yangu kwa wana Foroforo ni kufata miongozi iliyo letwa na wezetu wa tamisemi hatuongozwi na Halmashauri za vichwa vyetu kuna Halmashauri ya wilaya alafu kuna Halmashauri ya vichwa vyetu lazima tufate maelekezo ya tamisemi katika ujenzi wa miradi yetu”
Dc jokate ameyasema hayo wakati wa ziara yake akitembelea na kukagua matumizi ya fedha katika miradi mbalimbali ya elimu inayojengwa na wilaya ya Korogwe ambapo amesema kuwa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi katika miradi mbalimbali wilayani humo lengo likiwa ni kuendelea kutatua changamoto mbalimbali za zinazo wakabili wananchi, pia Mh Jokate Mwegelo ametembelea kata mnyuzi,makumba,magoma pamoja na foroforo
“sisi kama viongozi wa kata na vijiji na vitongozi tuna wajibu wa kumsemea Mhe.Rais kwa miradi mingi anayo leta kwenye maeneo yetu kwani miradi hii inayoletwa ina faidisha wananchi wetu”
Hata hivyo Jokate ametembelea kata mnyuzi,makumba,magoma pamoja na foroforo .