Mwenyekiti wa kampuni kubwa ya bidhaa za kusafisha majumbani nchini China amekejeliwa na watumiaji wa mitandao baada ya video inayomuonyesha akila kipande cha sabuni kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wafanyakazi, bosi wa Hongwei, mtengenezaji maarufu wa bidhaa za kusafisha iliyoanzishwa mwaka wa 1952, alisikika akitoa uwasilishaji wa namna sabuni hiyo ya kufulia ilivyonzuri, akiwaambia watu kwamba haina vitu vyenye madhara, bali alkali, mafuta ya wanyama, na maziwa.
Ili kushawishika iwezekanavyo, mwanamume huyo alichukua kipande cha sabuni na kuanza kukitafuna , kabla ya kuiweka kwenye maji.
“Hakuna vitu vyenye madhara,” bosi wa Hongwei anasema kwenye klipu fupi . “Ina ladha ya mafuta ya ng’ombe na kondoo na maziwa. “Hakuna madhara inapoingia ndani ya mwili wako, itaondoa mafuta na uchafu mwilini.”