Manchester united imethibitisha kwa kusema “Tangu madai yalipotolewa kwa mara ya kwanza mwezi Juni, Antony ameshirikiana na uchunguzi wa polisi nchini Brazil na Uingereza, na anaendelea kufanya hivyo”. “Kama mwajiri wa Antony, Manchester United imeamua kwamba ataanza tena mazoezi Carrington, na atapatikana kwa ajili ya kuchaguliwa, wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea. Hili litawekwa chini ya uangalizi ikisubiri maendeleo zaidi katika kesi hiyo”.
“Kama klabu, tunalaani vitendo vya unyanyasaji. Tunatambua umuhimu wa kuwalinda wale wote wanaohusika katika hali hii, na tunakubali athari zinazotokana na tuhuma hizi kwa waathirika wa unyanyasaji”.