Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore, amesema suala ya kufanyika kwa uchaguzi sio kipaumbele kwa sasa ikilinganishwa na usalama.
Matamshi ya kiongozi huyo wa kijeshi yanakuja wakati huu ikiwa imepita mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani kupitia njia ya mapinduzi.
Traore alikuwa ameahidi kurejelewa kwa demokrasia na uchaguzi urais kufikia Julai 2024.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu suala hilo tata la uchaguzi ambapo amesema kwa sasa anahitaji kushugulikia tatizo la usalama katika nchi iliyokumbwa na ghasia za wanajihadi.
Baadhi ya raia wa Burkina Faso wamekuwa wakishinikiza kufanyika kwa marekebisho ya katiba