Serikali Mkoani Morogoro imekabdhi msaada wa zaidi ya milioni 50 Kwa waathirika wa mafuriko Wilayani kilosa Mkoani humo ikiwemo ,chakula,mavazi na vyombo .
Akikabithi msaada huo Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amesema baada ya kutokea changamoto hiyo wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali imechanga fedha na kununua mahitaji mbalimbali Ili kuwasaidia waathirika hao Kwa kipindi ambacho utaratibu mwingine unasubiriwa
Mhe. Adam Kighoma Malima amesema wananchi zaidi ya 4700 wameathiriwa na mafuriko hayo huku nyumba 997 zilizingirwa na maji kati ya hizo nyumba 85 zimesombwa na maji kabisa.
Rc Malima amesema mafuriko hayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja manne, Barabara na mashamba vyakula na mali nyingine huku watu wawili wakiripotiwa kufariki kutokana mafuriko
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameishukuru Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa, Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya pamoja na wadau waliotoa misaada hiyo na kwamba Serikali inawajali wananchi wake.
DC Shaka amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi bilioni 13 kwa ajili kuboresha miundombinu ndani ya Wilaya hiyo kwa lengo la kupunguza maafa huku akibainisha kuwa waathirika hao bado wanauhitaji wa misaada hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia waathirika wa mafuriko hayo.
Akizungunza Kwa niaba ya wadau ,Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Bi. Janeth shango kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa benki hiyo ametoa pole kwa wananchi waliyoathirika Wilayani Kilosa ambapo benki hiyo imetoa shilingi milioni 10.
Bi.Janeth amebainisha kuwa Benk hiyo ina utaratibu wa kutoa kwa wananchi sehemu ya faida wanayoipata hususan kwa waliopatwa na matatizo mbalimbali ili kuungana na Serikali katika kupunguza matatizo kwa wananchi hao.