Vyombo vya habari vya Israel vimenukuu vyanzo vya jeshi la Israel vikisema kuwa jeshi liko tayari kuivamia Rafah kusini mwa Gaza katika muda wa saa 72 iwapo hakuna makubaliano ya kusitisha mapigano yatafikiwa.
Misri inaandaa mazungumzo ya kina na wajumbe kutoka Israel na Hamas yenye lengo la kufikia usitishaji vita huko Gaza.
Tovuti ya habari ya Israel ya Ynet iliripoti kuwa Mkuu wa Majeshi ya Israel Herzi Halevi aliidhinisha mipango ya mwisho ya mashambulizi ya kijeshi huko Rafah pamoja na mpango wa kuwahamisha raia kuelekea maeneo ya katikati mwa Gaza.
Tovuti ya habari ilinukuu chanzo ambacho hakikutajwa jina kwamba vifaru na wanajeshi wa jeshi la Israel wamejipanga karibu na mpaka wa Gaza, na tayari kwa mwanga wa kijani kuanza mashambulizi.
Imeongeza kuwa saa 48 hadi 72 zijazo ni muhimu katika kufikia makubaliano na kundi la Hamas au kuanzisha mashambulizi dhidi ya Rafah.