Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Katika hotuba yaka amesisitiza umuhimu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Akili Bandia (Artificial Intelligence) kwa maendeleo ya elimu na dunia kwa ujumla.
Amesema kuwa dunia inabadilika na kuhamia kwenye teknolojia za kisasa, na kuwashauri wanafunzi kutumia fursa ya kitengo cha TEHAMA kilichopo shuleni humo kwa kujifunza kwa undani teknolojia hizo.
“Dunia sasa imehamia kwenye Akili Bandia, au Akili Unde kama ninavyopenda kuiita. Hatutatumia tena kalamu na karatasi kwa kiasi kikubwa, mambo mengi yatakuwa yanafanyika kwenye mitandao,” amesema Rais Samia.
Rais Samia aliendelea kwa kusema kuwa majibu ya maswali mengi ya kitaaluma yanapatikana mitandaoni, akiwahimiza wanafunzi kutumia zana kama Google na ChatGPT kupata majawabu ya masomo yao. “Mkijifunza vizuri, mtaona siri ya majawabu yote iko mitandaoni, mnapaswa kutumia fursa hiyo ipasavyo,” Rais Samia