Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali Wachimbaji wote na wafanyabiashara wa madini ambao hawatafuata Sheria ya Madini na kujiingiza kwenye utoroshaji wa madini, ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni, kutaifisha mali zao na kutoruhusiwa kufanya tena biashara ya madini hapa nchini.
Amesema hayo Novemba 16, wakati akifungua Mkutano wa Viongozi na Kamati Tendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Karemjee, Jijini Dar es Salaam.
Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania FEMATA Ndg. John Bina amesema mkutano wao huo unafaida kubwa kwao kwakuwa unakwenda kutathmini mambo mbalimbali kwa faida ya Shirikisho lao ikiwemo pia fursa na kufahamu kwanamna ipi wanatatua changamoto zao.
Hata hivyo amesema Viongozi wa wachimbaji lazima awe mchimbaji na wamekuja hapo wana mambo yanayotakiwa kushauri Serikali na mengine nini wafanye mipango na maoni hadi mwaka 2025 kuangalia maslahi mapana ya sekta yao.
Miongoni mwa ajenda ni kuwajenga viongozi waliochaguliwa ili waweze kukidhi mahitaji ya uongozi, kubuni vyanzo vya mapato FEMATA ,kuangalia muunganiko wa vyama vyote ili wawe na sauti ya pamoja ,Kujadili namna yakudhibiti makundi ya whatsap ,kuangalia majukumu ya viongozi wa wachimbaji na Serikali hasa wizara ya madini ,namna ya usemaji ngazi matawi mpaka taifa ,Katiba ya FEMATA ,Changamoto ya uwekezaji kutoka nje ,mahusiano ya wachimbaji pamoja na wizara ya TAMISEMI ,Kuishauri serikali wakati wa B.O.T kununua dhahabu ,Changamoto za Tanzanite na almasi ,mchakato wa Benki ya wachimbaji, Ruzuku kutoka Serikali kwaajili ya kusaidia vyama ,Soko la Afrika madini kuwa Tanzania na mengineyo
Vilevile, Ndg, Bina amewataka wachimbaji wadogo kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kujenga na sio kulumbana na kujadiliana mambo ya msingi kwa kuwa shirikisho hilo ni la kibiashara na kwamba matarajio ya serikali kwa sasa ni kuona FEMATA inapiga hatua kubwa huku wanachama kuwa njia moja.