Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Julius Kimario maarufu kwa Babuu mkazi wa mtaa wa Mianzinii katika kata ya Kiranyi wilayani Arumeru Mkoani Arusha amekutwa na chupa 70 ambazo ni zaidi ya lita mia moja pamoja na ndoo za kinyesi sitaa huku akidai kwamba amezihifadhi kwenye chumba hicho anachoishi kwa miezi minne
Julius anayejishughulisha na kazi ya ufundi wa maturubai ambaye amezua taharuki katika eneo hilo amesema kuwa watu wanashangaa lakini hajihusishi na imani za kishirikina
“Hiyo haina shida yeyote sio imani za kishirikina wao ndio wanaoamin,nimejisaidia kwa kipindi cha miezi minne yale ni maji machafu yamechanganyika na kinyesi”
Wananchi wa eneo hilo walifika katika chumba hicho nakukuta kijana huyo akiwa analala chini huku vitu mbalimbali vikikutwa chumbani kama fedha za zamani,vitabu mafuta huku wakimtaka ahame eneo hilo