Mohamed Salah anataka kusaini mkataba wa miaka mitatu kusalia Liverpool, hii ni kutokana na ripoti mbalimbali za ulingo wa michezo huku majadiliano kuhusu mustakabali wa winga huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa yakifikia hatua muhimu.
Huku Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri akimaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, Salah anataka mkataba mpya utakaodumu hadi 2028.
Ni wakati muhimu pia kwa Virgil van Dijk, huku Nicolo Schira akiripoti kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.
Beki wa kati wa Uholanzi na Liverpool wakijaribu kuongeza mkataba wake hadi 2027.