Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew ametoa Rai kwa wadau kushirikiana na mamlka za maji pamoja na watendaji wake ili kubuni mbinu mpya zitakazoongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi zitakazosidia kukabiliana changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama
Rai hiyo ameitoa Mkoani Morogoro katika kongamono lililowakutanisha wadau wa maji liloandaliwa na jumuiya ya watumia huduma za maji nchini (ATAWAS) Lenye lengo la kujadiliana namna bora ya kutimiza malengo ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama ifakapo2030.
Aidha Naibu waziri wa maji ametoa rai kwa watendaji wa mamlka za maji katika Kuelekea kipindi cha mvua kufanya maboresho ya miundombinu ya maji .
Kwa upande wake Mhandisi Geoffrey Hilly – Mwenyekiti bodi ya ATAWAS amesema kuwa dhumuni kuu la mkutano huu uliofanyika Mkoani Morogoro ni kuona kwamba namna ya kushirikiana na wadau mbalimbali kupata urahisi wa biashara/Fedha ya miradi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
Aidha Mhandisi Patrick Nzamba ambaye ni Mwenyekiti wa wakurugenzi watendaji wa mamlaka za maji ameushukuru uongozi wa mamlaka za maji kwa kusimamia na kutekeleza mipango ambayo wamejiwekea
Pascal Elias ni mmoja wa wakazi wa Morogoro ambapo amesema Serikali kushirikiana na wadau waendelee kuwa pamoja Ili hufuma hiyo ipatikane.
Amesema kipindi cha kiangazi huduma hiyo imekuwa changamoto hivyo ni lazima kuweka mipango ya muda mrefu.