Justine Magembe(30) kada wa CCM mkazi wa Ikomwa Manispaa ya Tabora anadaiwa kujiua kwa kunywa Sumu baada ya mgombea aliyetarajia kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa, Vijiji na vitongoji kushindwa uchaguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ,ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ulinzi na usalama mkoa akiwa katika kikoa cha wadau wa zao la Tumbaku na wakulima ameelezea tukio hilo na kusema marehemu huyo baada ya kuona upande wa upinzani umeshinda na hakuwa anamtaka mtu huyo akaona ni vyema ajiue kuliko kuongozwa na mtu asiyempenda.
“Chaguzi zimeisha jana na matokeo yametangazwa na Mh Waziri wa Tamisemi,sisi hapa jana tulipata tukio la mmoja wetu aliyekuwa mpambe kama mlivyokuwa ninyi akafariki kwa sababu umeshinda upinzani mtaani kwake ameshinda mtu ambaye hamtaki kwahiyo akaona anywe sumu yakunyunyizia kwenye tumbaku madaktari walijaribu kumuokoa lakini ikashindikana’’RC CHACHA.