Pep Guardiola amedokeza kuwa atajaribu kuinoa timu ya taifa atakapoondoka Manchester City.
Guardiola hivi majuzi alimaliza uvumi juu ya mustakabali wake kwa kusaini kandarasi mpya mbili na City, ambapo amekuwa tangu 2016.
Raia huyo wa Catalunya amejitolea kuitumikia City hadi mwisho wa msimu wa 2026/27, lakini mwenendo mbaya wa timu hiyo kwa sasa umechochea uvumi mill kwa mara nyingine tena.
City wameshinda mechi moja kati ya tisa za mwisho katika michuano yote na wameteleza kwa pointi nane nyuma ya vinara wa Premier League, Liverpool, ambao pia wana mchezo mkononi.
Guardiola ameonyesha dalili za mfadhaiko wakati wa kushuka kwa kiwango kikubwa na ameibua sintofahamu kwa kujadili waziwazi nia yake ya kuboresha ustadi wake wa Kifaransa, kupika na gofu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 pia alithibitisha nia yake ya kubadilika kutoka kwa kandanda ya vilabu hadi usimamizi wa timu ya taifa wakati wa kuondoka City utakapofika.
“Wakati utakuja ambapo ninahisi inatosha na bila shaka nitaacha,” Guardiola alimwambia mpishi Dani Garcia kwenye chaneli yake ya YouTube ya Desmontadito.
“Sitasimamia timu nyingine. Sizungumzii juu ya siku zijazo za muda mrefu lakini sitachofanya ni kuondoka Manchester City na kwenda nchi nyingine kufanya kama nilivyo sasa.