Israel yathibitisha utambulisho wa miili yote 4 iliyokabidhiwa na Hamas
Rais wa Israel Isaac Herzog amethibitisha kuwa utambulisho wa miili yote minne ya mateka umethibitishwa.
Ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti mapema jinsi utambulisho wa miili ikiwemo Shlomo Mansour, Itzik Elgarat na Ohad Yahalomi ulivyothibitishwa.
Israel sasa imetambua mabaki ya Tsachi Idan.
“Kurejeshwa kwa miili ya ndugu zetu kutoka utumwani kunasisitiza wajibu wa kufanya kila tuwezalo kuwarudisha mara moja wale wote waliotekwa nyara kutoka kuzimu ya utumwa huko Gaza,” Herzog alisema.
Gazeti la Israel la Haaretz liliripoti kuwa Wapalestina 43 waliokuwa wanazuiliwa huko Ofer wamehamishiwa kwenye Shirika la Msalaba Mwekundu.
Kikundi kilishuka kwenye basi na kushangiliwa na mamia waliokusanyika nje, huku baadhi ya wanaume walioachiliwa – waliovalia koti za kijani kibichi na wakipandishwa juu na umati.
Takriban wafungwa 100 zaidi wa Kipalestina walikabidhiwa Misri, ambako watakaa hadi nchi nyingine iwakubali, ripoti za Reuters zikinukuu chanzo cha Hamas na vyombo vya habari vya Misri.
Magari ya kubebea wagonjwa baadaye yaliwasili katika hospitali ya Uropa iliyoko Khan Younis, kusini mwa Gaza, mapema Alhamisi ikiwasafirisha Wapalestina walioachiliwa huru, ambao wanatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Wafungwa walioachiliwa katika mabadilishano ya awali wamekatwa miguu na mikono wakiwa chini ya ulinzi wa Israel na wengi wao wamedhoofika sana.