Ni wajibu wetu kumsifia na kumpongeza binadamu yeyote ambae ana kiu na anayatafuta maendeleo kwa kasi, hiini good news nyingine kwa sababu Watanzania sasa hivi wanaanza ku-take over kwa wingi na kuvuka hata mipaka kwenda nje ya nchi tena kwa kufanya mambo makubwa tu.
Kutoka hapa Kampala ripota wako wa nguvu Bill The African nakupa hii kuhusu uzinduzi wa Azam Digital television iliyosheheni zaidi ya channel 50 za kitaifa na kimataifa za Tanzania na zisizo za Tanzania umefanyika Kampala Uganda na kusimamiwa na Makamu wa Rais wa Uganda aliemwakilisha Rais Museveni.
Azam TV ambayo itawaruhusu watu mbalimbali waliopo Uganda kutazama TV stations za Tanzania ikiwemo CloudsTV na Television nyingine.
Kuhusu nchi ya Uganda kuzungumza kiswahili kwa asilimia ndogo, balozi wa Tanzania Uganda Dr. Ladislaus Komba amesema ‘nimefurahi sana kwa sababu uwepo wa Tanzania utaongezeka, pia wanaleta changamoto kwa sababu soko la TV Uganda bado lina nafasi… Lugha ya Kiswahili nadhani itapata fursa na nafasi nyingine ya kuenezwa kwa haraka zaidi kwa kutumia Television hii’
‘Kiswahili kina historia yake kwa Waganda…. ni lugha ambayo zamani ilikua inatumika sana na Wanajeshi hivyo watu wengi waliokua wanawaogopa Wanajeshi walikua hawataki kuongea Kiswahili, kwa baadhi ya makabila hapa ilikua inajulikana kama lugha ya wahuniwahuni na wageni lakini sasa hivi wameelewa kwamba ndio lugha inaweza kutuunganisha Afrika Mashariki’
‘Tunatarajia kwamba Azam TV itasaidia kuongeza watu kujifunza Kiswahili, sasa hivi Waganda wameshagundua umuhimu wa Kiswahili na mpango wa lugha hii kufundishwa mashuleni, shule za msingi, sekondari mpaka chuo kikuu’ – Balozi Komba
Stori hii imekuja siku kadhaa baada ya good news ya Clouds Media Group kutangaza kufungua ofisi zake chini ya Clouds TV International huko Abu Dhabi falme za kiarabu itakayoanza kwa kuhudumia nchi hizo na Kingston Jamaica.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB