Hekaheka ya leo inahusu stori iliyopo mtaani kuhusiana na jamaa ambaye anajiita ‘Maalim’, ameshika sana dini na ametumia kivuli cha dini kulaghai wanawake, anawaoa na baadaye anawaibia na kuwatelekeza.
Ndoa ya mwisho ya Maalim imeisha na ametoroka na seti ya vito vya dhahabu vya mke wake, na stori iliyopo ni kuwa amekuwa akiwaibia wanawake zake na kutokomea navyo.
Kwenye Hekaheka ya kesho utawasikia wanawake ambao bwana Maalim amewahi kuwaoa na kuwaacha kwa staili hiyo hiyo.
Kisikie alichokisimulia Geah Habib kwenye Intro ya Hekaheka hiyo ya leo kupitia 88.5 Clouds FM Dar es Salaam.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook