MTUHUMIWA wa kesi ya kulawiti mtoto wa kiume, aliyekua akitafutwa na mahakama ya rufaa Sixtus Kimaro ambaye alikutwa na tuhuma hizo wakati akiwa Padri katika kaniska katoliki jimbo kuu la Dar es salaam amefia nchini Msumbuji na mwili wake umesafirishwa kuja Dar.
Taarifa za kifo cha Padri huyo zililifikia Gazeti hili wakati tayari mwili wake ukiwa umefikishwa katika hospitali ya Jeshi JWTZ,Lugalo na baadaye zilithibitishwa na Askofu mkuu wa Jimbo Denis Wigilla.
Padri Wigila alisema taarifa za mazishi zinafanyika chini ya familia yake kwani tayari aliashaacha kazi ya Upadri hivyo kanisa halitahusika na taratibu za mazishi zitakazofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Julai mwaka huu Padri huyo alitoroka n chini baada ya kuhiukumiwa kifumngo cha miaka30 jela ambapo alikua na mashtaka matatu ikiwemo kumlawiti motto wa kiume wa miaka17,shambulio la aibu na kumdhalilisha mtoto huyo.
HABARILEO
Kamati ndogo ya Madiwani ya Halmashauri ya Arusha imegundua kuwa jiji hilo limekua likipoteza zaidi ya milioni60 kwa mwezi kutokana na uzembe wa kushindwa kukusanya ushuru mdogo wa masoko17 katika maeneo mbalimbali ya jiji humo.
Kamati ya madiwani watatu imegundua vyanzo 25 vyenye utata wa mapato ambapo mawakala hulipa ushuru mdogo wa mwezi au wafanyabiashara wanalipa kwa risiti ambazo jiji halina kumbukumbu sahihi.
Kamati hiyo iliteuliwa na Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo na kutakiwa kutafuta majibu kuhusu sababu za mapato ya jiji kupotea na hatua gani zichukuliwe kuongeza mapato.
Uzembe mwingine uligundulika na kamati hiyo iliyotumia siku tatu kujua matatizo hayo ni pamoja na wafanyabiashara wa soko la Mbunga ya chumvi kata ya Terat lenye ukubwa wa eka saba kufanya biashara bila kuwa na leseni.
Taarifa hiyo ilikua ikionyesha kuwa soko la Mbuga limekua likipoteza Zaidi ya milioni35 na wafanyabiashara wakifuatwa katika soko hilo hudai fedha za ushuru wanalipa kwa mwanasiasa mmoja ambaye hakuwekwa jina gazetini ambaye huwa hatoi stakabadhi.
MWANANCHI
Baadhi ya wananchi Mkoani Mbeya wameliomba Jeshi la polisi kwa kushirikiamna na Mamlaka ya usafiri wanchi kavu na majini Sumatra kufanya ukaguzi wa mabasi ya Mikoani kabla ya kuanza safari ili kukabiliana na changamoto ya ajali za barabarani hususani katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Baadhi ya abiria walisema madereva wamekua wakikiuka sheria za usalama barabarani kwa makusudi na hupunguza mwendo katika maeneo ambayo wamegundua kuwepo askari wa usalama.
“Madereva wana mbinu nyingi sana za kukabiliana na askari wa barabarani kwani mara nyingi tumekua tukishuhudia wakiomnyeshana ishara na katika hilo inabidi Jeshi la polisi na Sumatra kujipanga upya ili kuweza kuwadhibiti”alisema mmoja wa abiri.
Waliongeza kuwa ni vyema Serikali ikaweka adhabu ya kunyongwa kwa madereva wazembe ambao husababisha ajali kwa makusudi kwani itakua fundisho kwa wale wenye tabia hiyo na hatimaye kuondokana na ajali hizi kwa asilimia kubwa.
MWANANCHI
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wameshauri kujifunza lugha ya kichina ili kukabiliana na changamoto ya ajira.
Ushauri huo ulitolewa na Profesa Henry Muzale kutoka katika kituo kinachojihusisha na mafunzo ya lugha ya kichina akisema hivi sasa Taifa la China linazidi kupiga hatua za kimaendeleo hivyo wanafunzi watumie fursa hiyo ili kuweza kupata ajira kirahisi.
“Sasa hivi kampuni nyingi za kichina zinakuja kuwekeza hapa nchini,na baadhi ya wamiliki wanajua lugha ya Kichina,itakua njia rahisi kwa wanafunzi wetu wanaohitimu kupata ajira kwenye kampuni hizo”alisema Profesa Muzale.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa bure kwa kipindi cha mihula sita na kwamba hadi sasa Zaidi ya wanafunzi700 kutoa chuo hicho wamejiunga na kozi hiyo.
JAMBOLEO
Katika kujidhatiti na kuimarisha jeshi la anga nchini Rwanda,Rais Kagame amenunua makombora aina ya TL50 yaliyotengenezwa nchini China.
Rwanda itakua nchi ya kwanza barani Afrika kumiliki makombora ya aina hiyo kutokana na teknolojia ya kisasa iliyotumika katika utengenezaji wake.
Makombora hayo yanauwezo wa kukabiliana na adui kutoka nchi kavu kwa umbali wa kilometa20 hadi30 pia yana uwezo wa kufikia ndege ya adui umbali wa kilometa50,hivyo kuwa makombora ya aina yake.
Katika jarida la Kanwa liliandika kuwa makombora hayo yaliyonunuliwa na Rwanda ni ya teknolojia ya hali ya juu ambayo mpaka sasa hakuna nchi yoyote ya Afrika iliyoweza kuwa nayo na imenunua kiasi kidogo tu cha makombora hayo.
MZALENDO
Wauguzi wa Zahanati ya Bonyokwa iliyoko Wilayani Ilala,Dar es salaam wanalazimika kutumia tochi au mishumaa kusaidia wajawazito wanaokwenda kujifungua nyakati za usiku kutokana na kutoweka kwa nishati ya umeme.
Hali hiyo inasababisha wauguzi kufanya kazi hiyo katika mazingira magumu ambapo wanaiomba Serikali kuharakisha umeme katika Zahanati hiyo.
Wauguzi hao walisema wamepelekewa taa za kuchaji ambazo kuna wakati zinasumbua na kulazimika kutumia mishumaa au tochi za simu.
Diwani viti maalum wa kata ya Bonyokwa Tumike Malilo alisema wajawazito kujifungulia gizani itabaki kuwa ni historia kwa kuwa Serikali inatarajia kufikisha nishati ya umeme katika Zahanati hiyo hivi karibuni.
MZALENDO
Juhudi za Serikali kutaka kubadili maisha ya jamii ya Wahdzabe ili waache kutegemea vyakula vya asili na kujiingiza katika kilimo zinakabiliwa na ugumu ikiwemo kutaka kupatiwa mchele ikiambatana na nyama ya nyani na tumbili ambacho ni chakula chao kikuu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida DK Perseko Kone aliwatembelea wananchi wa eneo la pori la Kipamba umbali wa Zaidi ya km120 Kaskazini Mashariki mwa mji wa Singida.
Kone aliitaka jamii hiyo kutumia misaada ya Serikali kwa lengo linalokusudiwa na kwamba uamuzi wao wa kubadilisha matumizi ya majembe haukubaliki.
Mkuu huyo wa Mkoa aliambiwa kwamba majembe ya kulimia yaliyopelekwa na Serikali mwaka jana badala ya kuyatumia katika shughuli zilizokusudiwa waliyakata na kutengenezea mishale na visu kwa ajili ya uwindaji.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook