Ni siku ya 42 tangu kuanza kwa mashindano ya Big Brother Africa na idadi ya washiriki inazidi kupungua kadri siku zinavyozidi kusonga ambapo usiku wa Novemba 16 2014 washiriki wengine wawili wametolewa.
Aliyekuwa anaiwakilisha Afrika Kusini, Samantha pamoja na Achalume Malick a.k.a ‘Mr. Numbers’ au Mr. 265 mshiriki wa Malawi wametolewa kwenye Mashindano hayo.
Mr. 265 amesema mbali na ugumu wa mashindano hayo, ameinjoy kuwa ndani ya jumba hilo ambapo kwa upande mwingine baada ya hawa washiriki kutolewa kuna washiriki wengine 12 waliobakia ndani ya jumba hilo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook