Katikati ya Jiji la Nairobi kuna watu ambao wana asili ya kihindi, hawana makazi ya kuishi na wamekuwa wakiishi kwa kuombaomba.
Watu hao wamekuwa na maisha hayo mbali ya kuwa na ndugu.
Kijana mmoja amesema kuwa wazazi wake walikuwa walimu lakini wote walifariki na amekuwa akirandaranda katika eneo hilo kwabali ya kuwa na ndugu
Siku chache zilizopita walipata ajali ambapo baadhi ya vitu vyao viliungua kwa moto huku wakiwalaumu watu ambao wana asili kama yao wakidai kwamba wanaishi maisha ambayo yanawadhalilisha hata wao.
Hata hivyo majirani wameonekana kuwalaumu vijana hao kwa hali waliyonayo kwa kuwa waliwasaidia kupata kazi na kufanya kwa muda mfupi baadaye wakarudi tena eneo hilo.
Hii ni moja ya stori ambayo imevuta hisia za wengi hasa kutokana na asili walionayo jamaa hawa.
Hapa iko sauti niliyoirekodi taarifa hiyo wakati ikiripotiwa na kituo cha K24 cha Kenya.
Unaweza kuicheki stori hiyo pia kwenye video hii.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook