JAMBO LEO
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Dar, John Guinita na Mwenyekiti wa Chama hicho Singida, Mgana Msindai wameanga kumfikisha Mahakamani Mkuu mpya wa Wilaya ya K’ndoni, Paul Makonda kwa kuwatolea lugha za kashfa huku wakimtaka Rais Kikwete kutengua uteuzi wa DC huyo.
Guinita amesema amefikia uamuzi kenda Mahakamani baada ya Makonda kugoma kuwaomba radhi; “Tulimtaka Makonda atuombe radhina kufuta kashfa zake dhidi yetu kupirtia vyombovya habari kwa kwa wanasheria wetu.. Makonda alijibu kuwa ametumwa na chama na alikuwa anafanya kazi ya chama..”—Guinita.
Mwanasheria kutoka BM Attorneys amesema kisheria maneno ya Makonda ni ya udhalilishaji hivyo ni lazima achukuliwe hatu.
JAMBO LEO
Mmoja wa vigogo waliosimamishwa kazi Shirika la Ndege ATCL amesema kwamba katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Shirika hilo alikuwa na baadhi ya vigogo wengine waliopo kwenye idara nyeti lakini wenzake wamemgeuka.
“Mmoja ya viongozi hao (akamtaja) alichukua mgao wa kwanza Novemba19 mwaka 2014, .. mwenzetu alichukua dola 12,100 na Januari 19 mwaka huu akachukua tena dola 2,700”, amenukuliwa kigogo huyo.
“Tulikubaliana kuwa tutauificha menejiment kuhusu uchotaji huo wa fedha na kasha waowawashe moto kuishitaki Kampuni hiyo ya Kenya kwa kukiuka mkataba na kuidhalilisha kampuni yetu..”
Kigogo huyo anasema wenzake walimgeuka na kumfanya yeye mbuzi wa kafara wakati wanafahamu ukweli.
JAMBO LEO
Madiwani wa Manispaa ya Dodoma walilazimika kuvunja Kikao cha Baraza lao na kutoka nje kwenda kumwadhibu kibaka aliyeiba kofia za gari ya mtangazaji wa TBC, Victoria Patrick lililokuwa limeegeshwa nje ya Ukumbi wa Manispaa.
Kibaka huyo, Ladislaus Haule mkazi wa Kizota, alikurupushwa na kupewa kichapo kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa Polisi.
HABARI LEO
Kobe wadogo 250 wamekamatwa Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume wakiwa wanasafirishwa kwa njia ya magendo kwenda Malaysia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam amesema; “Tumekamatra kobe 250 wakiwa wamehifadhiwa vizuri katika masanduku yakiwa yameingizwa maembe ndani yake tayari kusafirishwa kwenda Malaysia”
Kamanda huyo amesema kwa sasa hawako tayari kumtaja mtuhumiwa kwa kuwa itaharibu upelelezi wao.
Kumekuwa na matukio ya wizi wa kobe kutoka Z’bar kwenda sehemu nyingine duniani ikiwemo Tanzania Bara ambapo wanyama hao wako kwenye orodhaya viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani nawanalidhwa na sheria za Kimataifa.
HABARI LEO
Ndege ya Jeshi la Wananchi JWTZ iliyokuwa katika mazoezi imeanguka jana na kuteketea moto huku rubani wake akiumia wakati akijiokoa Uwanja wa Ndege Mwanza.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi hilo Dar imesema ndege hiyo iliwaka moto baada ya ndege mnyama kuingia katika injini yake moja wakati ikiruka hivyo imeungua moto katika hali ya kawaida.
Ajali hiyo ilitokea wakati ndege hizo zikiwa kwenye mazoezi, Rubani Meja Peter Lyamunda alipoona ndege inawaka aliruka kwa kutumia vifaa maalum na hakupata jeraha kubwa zaidi ya kuumia mguu.
TANZANIA DAIMA
Vijana ambao wanadaiwa kuwa ni ndugu wa Mwalimu wa Kibasila, Gaudensia Albert aliyeishi na kinyesi kwa muda wa miaka miwili juzi walikwenda kudai vyombo vilivyokuwa vimehifadhi uchafu huo.
Mwenyekiti wa mtaa, Yahya Bwanga amesema; “Juzi usiku walikuja vijana kwenye Ofisi yetu ya Serikali ya Mtaa wakati mimi sikuwepo .. walimkuta mjumbe akawahoji wakaonekana wamekuja kuchukua vile vyombo vilivyokuwa na uchafu kwamba walitumwa na yule dada..”
Bwanga amesema waliwajibu kwamba vyombo vile havikuwepo kwa kuwa kazi ya kuteketeza uchafu huo ilifanywa na Manispaa.
“Hapa ndipo penye utata, juzi tumeambiwa kuwa yuko Muhimbili Muhimbii anapimwa akili leo tunaambiwaanadai vyombo vyake.. tumewaambia waende Manispaa..”—Bwanga.
Mwalimu huyo hakuweza kupatikana kwa kuwa tangu siku ya tukio hilo simu yake imekuwa ikiita bila kupokelewa.
TANZANIA DAIMA
Kauli ya Prof. Anna Tibaijuka kuwa shilingi mil. 10 ilikuwa hela ya mboga imezua gumzo kila mahali Dodoma ambapo kila kona ya kijiwe kulikuwa na mabishano na kila mmoja akisema lake kuhusu kauli hiyo wengine wakisema ni ya udhalilishaji wa Serikali na kuwadharau Watanzania.
“Kweli sasa Watanzania tunatakiwa kutambua kuwa hatuna viongozi na hizi sasa ndizo dalili tosha za kufanyika mabadiliko, haiwezekani kiongozi ambaye anatuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha bila aibu anasema kuwa sh. Mil 10 ni kwa ajili ya kununua mboga”—alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ally.
Dada mmoja mjasiriamali alisema; “ Inasikitisha kumuona dada mbunge huyo anavyowabeza Watanzania , sh. Mil. 10 akanunue mboga, mboga gani hiyo? Mimi hapa sijui kama nitakuja kuzipata katika maisha yangu..”—Catherine Mhinte.
TANZANIA DAIMA
Waziri wa Ujenzi Dk. Magufuli amefanya ukaguzi wa Kivuko kipya cha Mv Dar es Salaam kitakachofanya safari kutoka Dar kwenda Bagamoyo ambapo kitasaidia kuondoa kero ya usafiri inayosababishwa na foleni.
“Kivuko kimenunuliwa kwa fedha za Watanzania.. ni vema wakatumia rasilimali yao kwa kulipa hela kidogo na wakafaidika, pia wawahi sehemu zao za majukumu”—Dk. Magufuli.
Waziri Magufuli amesema Rais Kikwete atakizindua na ndani ya siku 10 mpaka 15 kitakuwa kimeanza kazi hukuakiahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokikabili kivuko cha Mv Magogoni.
MWANANCHI
Ujenzi wa majengo marefu kila kona ya Dar kunaliweka Jiji katika hali mbaya iwapo majanga yatatokea na hivyo kudaiwa kusababishwa maafa makubwa iwapo majanga yatatokea.
Katika kongamano lililofanyika kujadii ujenzi wa majengo na nyumba lililoandaliwa na Bodi ya Wahandisi, Profesa Kumbwaeli Salewi alisemahali sio nzuri Dar kutokana na ujenzi wa maghorofa pasipo kuweka maeneo ya maegesho ya magari, huku wengine wakisema kwamba maeneo kama ya Mitaa ya Samora na barabara ya Bibi Titi ilitakiwa kuwa maeneo ya wazi.
Wataalamu hao wameshauri kwamba weledi unahitajika ili madhara ya maafa yasiwe makubwa na pia kuangaliwa kwa mfumo wa utendaji ili kulinda watu na mali zao.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook