Nahodha wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi inaonekana ni miongoni mwa wazazi ambao wanaachia watoto wao wafanye au washabikie kile kitu ambacho wanakipenda.
Lionel Messi akihojiwa na TYC ameongea maisha ya familia yake na watoti wake kuwa mwanae akiwa anacheza nae nyumba alimtania baba yake kuwa yeye ni shabiki wa Liverpool kwa sababu wamemfunga baba yake.
“Tulikuwa tunacheza na mwanangu (Thiago) nyumbani akaniambia kuwa yeye ni shabiki wa Liverpool kwa sababu wamenifunga mimi”>>>>>Lionel Messi
Lionel Messi na mke wake Antonio wamebarikiwa kupata watoto watatu wa kiume Thiago, Mateo na Ciro lakini hivi karibuni Barcelona walitolewa nusu fainali ya Champions League na Liverpool baada ya kushinda 3-0 nyumbani na walipoenda Anfield wakafungwa 4-0.