Michezo

Simba watambulisha logo na jezi zao mpya (+picha)

on

Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara (VPL) Simba SC leo wamezindua jezi mpya sambamba na logo ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika 2020/21.

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema timu hiyo imejipanga kuhakikisha Simba inaendeshwa kiueledi huku ikizingatia misingi ya kibiashara ili kuvutia makampuni mengi kuwekeza kwao.

Pia Simba imethibitisha kumsajili mshambuliaji Charles Ilamfia ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea KMC.

“Kocha wetu alipomuona uwanjani Charles Ilamfia akauambia uongozi msajilini huyu kijana, miguu yake itatupa kitu Msimbazi, ni tumaini la baadae katika soka la nchi hii hususani upande wa washambuliaji, tumemsajili mshambuliaji toka KMC” Matola

LIVE: YANGA WAIBUKA NA JIPYA JUU YA MORISSON, WATOA TAMKO

Soma na hizi

Tupia Comments