Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesitisha zoezi la ubomoaji wa Hoteli ya Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ambayo inadaiwa kujengwa kwenye chanzo cha maji baada ya kuenea kwa uvumi kupitia kwenye mitandao ya kijamii kwamba itavunjwa.
Chalamila ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea eneo la uwekezaji wa Mbunge huyo ambapo amemwambia uamuzi huo ni maagizo kutoka kwa Rais John Magufuli kumruhusu Sugu kuendelea na shughuli zake za uwekezaji kama kawaida.